Alhamisi , 31st Mar , 2022

Kikao cha Halmashauri Kuu ya CCM Taifa kimependekeza jina la Katibu Mkuu wa zamani Abdulrahman Kinana kuteuliwa kupigiwa kura za kuwa Makamu Mwenyekiti wa CCM Bara.

Katibu Mkuu wa zamani wa CCM Abdulrahman Kinana

Kikao hicho kimefanyika leo 31 Machi 2022 Jijini Dodoma, katika Ukumbi wa (White House).

Endapo atapita katika nafasi hiyo atachukua nafasi ya Philip Mangula, ambaye anamaliza muda wake.

Kinana mwenye umri wa miaka 70 alikuwa Katibu Mkuu wa CCM kuanzia mwaka 2012 hadi 2018. 

Mangula mwenye umri wa miaka 81, aliteuliwa katika nafasi hiyo mwaka 2012.

Zoezi la kupiga kura litafanyika kesho April 1, 2022 kwenye Mkutano Mkuu wa Chama hicho Jijini Dodoma.