Alhamisi , 22nd Jan , 2015

Katibu mkuu wa chama cha mapinduzi CCM Abdulrahaman Kinana amepokewa kwa mabango na wananchi wa kijiji cha Miwani jimbo la uzini wilaya ya kati mkoa wa Kunisi Unguja Zanzibar wakimuomba kuwatatulia kero mbalimbali.

Baadhi ya wakazi wa Miwani wakimpokea Kinana (hayupo pichani) kwa mabango

Katibu mkuu wa chama cha mapinduzi CCM Abdulrahaman Kinana amepokewa kwa mabango na wananchi wa kijiji cha Miwani jimbo la uzini wilaya ya kati mkoa wa Kunisi Unguja Zanzibar wakimuomba kuwatatulia kero mbalimbali za kijiji hicho, ikiwemo maji,barabara na huduma za afya, sanjali na kuingilia kati mgogoro wa kutoelewana baina ya mbunge na mwakilishi wa jimbo hilo la uzini.

Kufuatia malalamiko hayo katibu mkuu wa chama cha mapinduzi CCM, Abdulrahmani Kinana analazimika kuwauliza viongozi, juu ya kero hizo na namna ya walivyozitatua, ambapo ndugu Kinana anakili wananchi kudai ahadi za CCM na jinsi zisivyotekelezwa.

Mohamedi Khatibu ambaye ni mbunge wa jimbo la Uzini, anayedaiwa kutokuwa na maelewano baina yake na mwakilishi wa jimbo hilo, mheshimiwa Mohamedi Raza ambapo mheshimiwa Khatibu anapinga vikali kauli za wananchi na kusema yapo maelewano baina yao.

Akiwa katika mkoa wa Kusini Unguja,katibu mkuu huyo wa CCM ametembelea miradi mbalimbali ya maendeleo na kuzungumza na wananchi ambapo amesema kuwa ahadi zote za chama hicho zitatekelezwa na kama hazikutekelezwa watarudi kwa wananchi kuwaambia kwanini hawakutekeleza.