Alhamisi , 18th Jun , 2015

Katibu mkuu wa Chama cha Mapindzuzi CCM, Abdulrahman Kinana ameikosoa sheria ya utumishi wa umma na sheria ya manunuzi ya umma kuwa ni vichaka vya wala rushwa, urasimu na kuongeza gharama za miradi.

Katibu mkuu wa Chama cha Mapindzuzi CCM, Abdulrahman Kinana ameikosoa sheria ya utumishi wa umma na sheria ya manunuzi ya umma kuwa ni vichaka vya wala rushwa, urasimu na kuongeza gharama za miradi ambapo amesema mara baada ya bunge la awamu ya tano kuapishwa CCM itapendekeza kuondolewa na kufutwa kwa sheria hizo kwa manufaa ya umma.

Akihutubia mamia ya wakazi wa mji wa Bukombe mkoani Geita, kwenye mkutano wa hadhara katibu mkuu wa CCM amesema lengo la sheria hizo lililkuwa ni zuri lakini sasa imekuwa mzigo kwa wananchi hasa kwenye miradi ya umma.

Aidha ndugu kinana amewataka wana chama na wapenzi wa CCM, kuwa wakali juu wa watendaji na watumishi wa serikali, ambao wamekuwa wakibainika kuiba mali za umma, huku wakiundiwa tume na kamati za kuchunguza wizi wao, hata kwa mambo ambayo yako wazi kwa kisingizio cha utawala bora.

Akiwa wilayani Bukombe mkoani Geita katibu mkuu ametembelea soko la wauza samaki na dagaa katika kijiji cha Runzewe na kueleza wauza samaki hao kulipa ushuru toka jijini mwanza hadi Bukoba kwa kila halmashauri ya wilaya wanazopita kwa kuwekewa vizuizi, ambapo amewaagiza wakuu wa mikoa kuondoa vizuizi hivyo.