Aliyekuwa Makamu Mwenyekiti wa CCM Bara Abdulrahman Kinana
Hayo yamebainishwa mara baada ya Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan kuridhia ombi la Kinana kujiuzulu nafasi yake.
Katika majibu yake Mwenyekiti wa CCM amesema "Ni kweli nilipokuomba utusaidie kwa nafasi ya Makamu Mwenyekiti nilikuahidi utakaa muda mfupi kama ulivyoomba, na kwa kweli nilipenda uendelee kutusaidia lakini kwa kuwa umeomba sana na ahadi ni deni nalazimika kwa moyo mzito kuridhia kujiuzulu kwako".
Pia Mwenyekiti wa CCM amesisitiza kuwa Chama kitaendelea kutumia uzoefu na maarifa ya Ndugu Kinana kila itakapohitajika.