
Katibu Mkuu wa CHADEMA, John Mnyika.
Taarifa hiyo imetolewa na Katibu Mkuu wa Chama hicho John Mnyika, na kusema kuwa Wabunge wote waliotekeleza agizo la Mwenyekiti wa chama hicho Freema Mbowe, walizingatia kanuni na namna bora za kujikinga kupata maambukizi ya Virusi vya Corona.
"Wabunge wetu wote ambao walitekeleza makubaliano na uamuzi wa chama wa kujitenga kwa siku 14, leo watarejea Bungeni kuendelea na shughuli za kuwawakilisha wananchi, huku wakiendelea kuzingatia tahadhari zote za kujikinga na kuwakinga wengine" amesema Mnyika.
Ikumbukwe kuwa Wabunge hao waliamua kujiweka karantini, baada ya kuwepo kwa taarifa za maambukizi ya Virusi vya Corona katika maeneo ya Bunge.