Jumapili , 27th Apr , 2014

Rais Jakaya Kikwete ametunukia nishani ya kumbukumbu ya miaka hamsini ya muungano, kwa watu mashuhuri nchini wakiwemo marais wastaafu, waasisi wa muungano pamoja na wake wa waasisi hao.

Rais wa Tanzania Dkt Jakaya Mrisho Kikwete, akimtunuku nishani ya muungano, rais mstaafu Benjamin William Mkapa

Waliotunukiwa nishani hizo ni waasisi wa muungano marehemu sheikh Abeid Amani Karume, mwalimu Julius Kambarage Nyerere pamoja na wake zao, Mama Fatuma Karume na mama Maria Nyerere.

Wengine waliotunukiwa nishani hizo ni marais wastaafu Ali Hassan Mwinyi, Benjamin Mkapa, waziri mkuu mstaafu na aliyekuwa mwenyekiti wa tume ya kurekebisha katiba Jaji mstaafu Joseph Warioba pamoja na mwenyekiti mtendaji wa makampuni ya IPP Dkt Reginald Mengi.