Alhamisi , 25th Mei , 2023

Jovin Godlove kijana (19) mkazi wa Kijiji cha Nduruma amekutwa ameuawa katika mazingira ya kutatanisha eneo la Njiro jijini Arusha, huku ndugu wa karibu wakisema kijana huyo kabla ya kifo chake alipotea kwa muda wa wiki mbili akiwa na msichana aliyesadikika kuwa ni mpenzi wake.

Jovin Godlove

Aidha ndugu hao wamesema kuwa Aprili 27 mwaka huu kuna watu walifika nyumbani wakimuulizia Jovin huku wakilalamika kwamba wakimshika watajua wao ni akina nani kwani kijana huyo ana mahusiano na mtoto wao.

Kwa upande mwingine wakazi wa kijiji hicho wanatoa rai kwa Jeshi la Polisi mkoani humo kuendeleza juhudi za kupambana na vitendo vya kkatili ili kuzuia taharuki kwenye jamii.

Aidha juhudi za kuwasiliana na uongozi wa  jeshi mkoani humo hazikufanikiwa baada ya kumtafuta Kamanda wa Jeshi la Polisi bila mafaniko.