Jumanne , 30th Jun , 2015

Suala la upungufu wa mafuta katika baadhi ya vituo nchini Tanzania limeibuka tena leo bungeni baada ya mbunge wa Ubungo Mh. John Mnyika kutaka bunge liahirishe shughuli zake ili kujadili suala kama suala la dharura.

Naibu waziri wa Nishati na Madini Mh. Charles Mwijage akisisitiza Jambo bungeni.

Mh. Mnyika amesema majibu ya serika ya jana kuwa hakuna uhaba wa mafuta ni ya uongo kwa kuwa jana wakati akielekea Bungeni Dodoma amethibitisha vituo zaidi ya nane vikiwa havina mafuta.

Mh. Mnyika amesema kuwa baadhi ya mikoa ukiwemo msoma umeonyesha dhahiri ukiwa na tatizo hilo lakini pia imegundulika hata baadhi ya vituo vinavyouza mafuta hayo vimepndisha bei kiholela hali inayowaathiri wananchi.

Wakijibu suala hilo Mawaziri wa Wizara zinazohusika na suala hilo akiwemo Naibu waziri wa Nishati na Madini Mh. Charles Mwijwage na Naibu Waziri wa Wizara ya Fedha Adam Malima, wamesema serikali inalitambua suala hilo na wameshachukua hatua na wanaendelea kufuatilia kwa ukaribu.

Waziri Mwijage amesema kuwa ni kweli kulikuwa na vituo ambavyo walivipitia na walivikuta havina mafuta lakini ameitaka Mamlaka ya Udhibiti wa Nishati na Maji EWURA, kushirikiana na Serikali kasaidia kutatua tatizo hilo

Akihitimisha hoja hiyo Naibu Spika wabunge la Jamhuri Mh. Job Ndugai amewataka wabunge kuwa watulivu na kusema hilo ni suala mtambuka ambalo anauhakika hadi kufikia kesho litakuwa limetatuliwa na kuwataka EWURA kutangaza bei mpya ya bidhaa hiyo kwa kuwa ndiyo utatuzo pekee wa suala hilo.