Jumamosi , 3rd Oct , 2020

Jamii imetakiwa kuacha kuhusisha ugonjwa wa kichaa cha Mbwa na imani za kishirikina, badala yake mtu anapong’atwa na mnyama huyo awahi hospitali kupata matibabu, kwani takwmu zinaonesha bara la Asia na Afrika ndiyo wanaongoza kwa ugonjwa huo.

Picha ikionesha mkono uliojeruhiwa na Mbwa.

Akizungumza na EATV jijini Dar es Salaam wakati wa mahojiano, mtaalamu wa afya ya jamii kutoka Wizara ya Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia ,Wazee na Watoto, Jubilate Bernard amesema wapo watu katika jamii wanahusisha dalili za ugonjwa huo na mambo ya kishirikina kitu ambacho sio sahihi.

Jubilate amesema kuwa, “Siku ya kichaa cha mbwa  huadhimishwa kila Septemba 28, duniani ambapo jumuiya ya kitaifa inatoa elimu juu ya ugonjwa huo  kwa duniani nchi ya India inaongoza kuwa na ugonjwa na  kufuata bara la Afrika.

“Watu  5,9000  hupoteza maisha kutokana na ugonjwa wa kichaa cha mbwa  asilimi 96 ni Afrika na asilia  huku asilimia 36 ni Afrika, kwa Tanzania kunatakwimu za wanaokwenda hospitali mwaka  jana  watu walioripoti kung’atwa na mbwa ni  12,680  nchi nzima ,kati yao ni watu sita walifariki", ameongeza Jubilate