Miongoni mwa kesi hizo ni pamoja na Mbunge wa Kigoma Kusini David Kafulila, aliyekuwa mgombea ubunge Iringa Mjini Fredrick Mwakalebela, aliyekuwa Mbunge wa Kahama James Lembeli, aliyekuwa Mbunge wa Nyamagana Ezekiel Wenje na aliyekuwa Mbunge wa Kilwa Kaskazini, Murtaza Mangungu.
Tangu uchaguzi huo umalizike Oktoba mwaka jana, jumla ya kesi 221 zilifunguliwa kati ya hizo 53 ni za ubunge na 173 madiwani na jumla ya Sh bilioni tatu zinahitajika kukamilisha usikilizaji wake.
Aidha washtakiwa wengine katika kesi hiyo mbali na washindi wa ubunge ni pamoja na Mwanasheria Mkuu wa Serikali na Msimamizi wa Uchaguzi katika jimbo husika. Hivi karibuni, Jaji Mkuu Mohamed Othman Chande alisema tayari mahakama hiyo imejipanga kumaliza kesi zote za uchaguzi hadi Juni mwaka huu, na imejipanga kusikiliza kesi 20 za wabunge.





