Alhamisi , 30th Jun , 2022

Kesi namba 12 inayomkabili Diana Bundala maarufu kama Mfalme Zumaridi na wafuasi wake 84 imekwama kuendelea leo katika Mahakama ya hakimu mkazi mkoa wa Mwanza kutokana na shahidi kupata changamoto ya kiafya.

Mbele ya hakimu mkazi mfawidhi wa mahakama ya hakimu mkazi mkoa wa Mwanza Monica Ndyekobora wakili upande wa serikali Emmanuel Luvinga ameiambia mahakama hiyo kuwa shahidi hiyo ambae ni askari wa jeshi la Polisi anayefahamika kwa jina la Evodius ana changamoto ya kiafya na kuomba ipangwe tarehe nyingine ya shauri hilo kuendelea kusikilizwa

Jopo la mawakili upande wa utetezi likiongozwa na wakili Erick Mutta likaridhia ombi hilo ndipo mahakama ikapanga tarehe ya kusikiliza shauri hilo ambayo ni Julai 13 huku shahidi akitakiwa kufika Mahakamani hapo bila kukosa ili kutoa Ushahidi wake

Inaelezwa kuwa Zumaridi na wafuasi wake 84 wanakabiliwa na kosa la kumshambulia askari Polisi ajulikanaye kama Jmaes Mgaya katika sehemu mbalimbali za mwili wake na kumzuia kutekeleza majukumu yake ya kazi mnamo February 23 mwaka huu katika eneo la Buguku, Buhongwa wilayani Nyamagana jijini Mwanza.