Mbunge wa Iringa Mjini kupitia CHADEMA, Mchungaji Peter Msigwa.
Hayo yamejiri leo Juni 5, 2020, wakati wa mahojiano maalum na EATV&EA Radio Digital, ambapo pia alikataa suala la yeye kumkimbia muigiaji Steve Nyerere, ambaye alishatangaza nia ya kugombea Ubunge Iringa Mjini.
"Ni kweli nimepeleka barua siku ya jana, mimi sijasema kwamba nataka kuwaaga wananchi wa Iringa hayo ni maneno yako, halafu ukisema nataka kumkimbia Steve Nyerere kwani yeye ni nani, na ndani ya siku nne nitaongea na vyombo vya habari kueleza kwanini naitaka nafasi hiyo" amesema Mchungaji Msigwa.
Juni 3, 2020 Katibu Mkuu wa CHADEMA John Mnyika alitangaza rasmi kufungua mlango wa watia nia ya kugombea nafasi ya Urais, waanze kupeleka barua ofisini kwake, zoezi ambalo litahitimishwa Juni 15, 2020.
