Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi Taifa, Abdulrahman Kinana
Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi Taifa, Abdulrahman Kinana ametoa taarifa hiyo mjini Dodoma, baada ya kutembelea na kukagua maendeleo na maandalizi ya ukumbi ambao utatumika na wajumbe wa mkutano mkuu maalumu wa CCM.
Kinana ametoa ratiba ya Mkutano huo ikiwemo ni pamoja na kupitisha jina moja la mgombea uenyekiti wa Chama hicho lakini pia ni pamoja na kupitsha ratiba ya Mkutano mkuu wa Chama.
Katibu Mkuu huyo amesema kuwa jina litakalopitishwa kwa ajili ya kugombea nafasi hiyo ya Uenyikiti ni moja tu la Rais wa Tanzania John Pombe Magufuli, na baada ya hapo kamati kuu itapeleka mapendekezo yake kwa Halmashauri kuu ya taifa.