
Mwenyekiti wa CHADEMA Freeman Mbowe
Akionge na EATV&EARadio Digital msemaji wa Chama hicho Tumaini Makene Leo Agosti 2, 2020 ameeleza kuwa mapendekezo yatakayo tolewa na kikao hicho kwa mujibu wa katiba ya chama hicho yatawasilishwa kwenye kikao cha Baraza Kuu kitakachofanyika kesho Agosti 3, 2020.
"Kamati kuu inakaa kuandaa kwa mujibu wa katiba ya chama kamati kuu inafanya utafiti wa majina ya wagombea urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Zanzibar kupitia Kamati Kuu Zanzibar itaanda ajenda kwa ajili ya kupeleka mapendekezo kwenye kikao cha Baraza Kuu".
Kikao hicho cha Kamati Kuu ya CHADEMA kinafanyika katika ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es salaam.