Waziri wa maendeleo ya mifugo na uvuvi Dkt Titus kamani
Wananchi wanaojishughulisha na ufugaji wa kuku katika mikoa ya kanda ya kaskazini wamelalamikia uingizaji wa vifaranga na kuku wa nyama kutoka nje ya nchi.
Wafugaji hao wakitoa kilio chao kwa Waziri wa maendeleo ya mifugo na uvuvi Dkt Titus kamani, wamedai kuwa licha ya tatizo hilo kuwaathiri kiuchumi linaweza kuhatarisha afya za walaji .
Wajasiriamali hao wametoa malalamiko yao kwa waziri wa mifugo Dkt Titus Kamani aliyetembelea baadhi ya miradi ya wananchi hao wilayani Arumeru mkoani Arusha .
Akizungumzia tatizo hilo waziri Kamani amewaomba wananchi kusaidiana na serikali kuwafichua watu hao kwani wanachofanya ni uhalifu na pia amewataka kuendelea kuelimisha jamii madhara ya matumizi ya bidhaa zinazoingizwa kwa njia za panya.
Uingizaji wa bidhaa kwa njia za panya ni miongoni mwa changamoto kubwa zinazoikabili mikoa ya kanda ya Kaskazini kutokana na kuwa na njia nyingi za panya ambazo pia zimekuwa zikitumika kuvusha bidhaa na vyakula kwenda nchi.