Alhamisi , 24th Aug , 2023

Jeshi la Wananchi wa Tanzania JWTZ limezitaka baadhi ya taasisi zinazowashonea watumishi wake sare zinazofanana na jeshi hilo pamoja na wafanyabiashara wanaoagiza sare hizo na wanaozivaa kuacha kufanya hivyo ndani ya siku saba kabla ya kuanza msako.

Kaimu Mkurugenzi wa habari na uhusiano makao makuu ya JWTZ Luteni Kanali Gaudentius Ilonda

Kaimu Mkurugenzi wa habari na uhusiano makao makuu ya JWTZ Luteni Kanali Gaudentius Ilonda, akitoa tahadhari hiyo mbele ya waandishi wa habari jijini Dodoma leo amesema baadhi wanaovaa mavazi hayo wamekuwa wakiyatumia kufanyia uhalifu na utapeli.

"JWTZ linawsihi na kuwaomba wananchi wote kusalimisha mavazi hayo ndani ya siku saba kuanzia leo na baada ya siku hizo kupita atakayekutwa nazo hatua kazi zitachukuliwa dhidi yake," amesema

Aidha Luteni Kanali ILONDA amesema licha ya wasanii wa Tanzania kuiletea mafanikio nchi lakini wanahusika na katazo hilo isipokuwa wanaweza kutumia mavazi hayo iwapo watakuwa wamepata kibali maalum.