Jumatatu , 6th Jun , 2016

Serikali ya Tanzania imeanzisha Jukwaa la uwezeshaji wanawake kiuchumi ambao utaratibu mazingira na shuguli za uzalishaji mali zinazofanywa na wanawake ili kuhakikisha dira ya kimataifa ya maendeleo endelevu ya usawa wa kijinsia na uwezeshaji wanawak

Makamu wa Rais Mama Samia akiwa pichani na kikundi cha watoto kilichoshiriki uzinduzi huo,

e unafikiwa kikamilifu.

Akizindua jukwaa hilo hii leo jijini Dar es salaam, Makamu wa rais mama Samia Suluhu Hassan amesema wanawake kote duniani huchangia wastani wa asilimia 50 ya jumla ya nguvu kazi ya kimataifa, endapo nguvu hiyo itatumika vuzuri wanawake watachangia dola trilioni 28 ya uchumi.

Mama Samia amesema, wanawake wengi bado wanakabiliwa na vikwazo katika masoko, upatikanaji wa raslimali, ubaguzi, unyonyaji na mila kandamizi hivyo jukwaa hilo litawakomboa kwa kuweka mifumo ya kisheria na mipango madhubuti ya kuelimisha na kuendeleza wanawake.

Jukwaa hilo litaratibiwa chini ya ofisi ya waziri mkuu pamoja na Wizara ya afya, maendeleo ya jamii, wazee na watoto ambapo kauli mbiu ya jukwaa hilo ikisema usinipe samaki nipe nyavu nikavue.