Ijumaa , 17th Jul , 2020

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt John Pombe Magufuli, amefanya uteuzi kwa Wakuu wa Wilaya na Mikoa hapa nchini, pamoja na Makatibu Wakuu na Manaibu ambao wataapishwa Jula 20, 2020, Ikulu ya Chamwino mkoani Dodoma.

Poichani ni Rais Magufuli, na viongozi wengine ambao amewatengua nafasi zao, akiwemo Profesa Mkumbo, Patrobas Katambi, Profesa Adolf Mkenda na Christopher Ole Sendeka.

Uteuzi huo umefanyika hii lo Julai 17, 2020, ambapo miongoni mwa aliowateua yupo Jumanne Fhika kuwa Mkuu wa Mkoa wa Njombe, ambapo kabla alikuwa Ofisi ya Rais na anachukua nafasi ya Christopher Ole Sendeka, mwingine ni Dkt Aloyce Nzuki aliyeteuliwa kuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utali akichukua nafasi ya Profesa Adolf Mkenda.

Mbali na hao Rais Magufuli, amewateua Mhandisi Anthony Sanga, kuwa Katibu Mkuu Wizara ya Maji, akichukua nafasi ya Profesa Kitila Mkumbo, ambapo kabla ya uteuzi huo Mhandisi Sanga alikuwa ni Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji, pia amemteua Dkt Allan Kijazi kuwa Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii, huku pia Dkt Allan ataendelea kuwa Kamishna wa Uhifadhi wa TANAPA.

Wengine walioteuliwa hii leo ni Fadhili Mohamed Juma kuwa Mkuu wa Wilaya ya Geita, akichukua nafasi ya Josephat Paulo Maganga, ambaye ameteuliwa kuwa Mkuu wa Wilaya ya Dodoma akichukua nafasi ya Patrobas Katambi.