
Rais Magufuli ameyasema hayo leo jijini Dodoma wakati anafungua mkutano wa Jumuiya ya Wazazi wa CCM ambao ni mwendelezo wa mikutano ya uchaguzi wa Jumuiya mbalimbali za Chama hicho.
“Jumuiya hii ilianza mwaka 1955 ikiwa inaitwa Tanganyika African Parent Associations (TAPA), na aliyeianzisha ni Baba wa taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere na anafahamu kwanini ilianza nikiifuta nitakuwa nimekosa busara na nitalaaniwa”, amesema Rais Magufuli.
Aidha Rais Magufuli ameongeza kuwa “Napenda niwahakikishie Jumuiya hii itaendelea kusimama kama zilivyo Jumuiya zingine ndani ya Chama”, ameongeza.
Aidha Rais magufuli amesifu mafanikio mbalimbali ambayo yamekuwa yakifanywa na Jumuiya hiyo ikiwemo kumiliki shule mbalimbali pamoja na Chuo cha sanaa cha Kaole kilichopo Pwani. Mkutano huo unatarajiwa kufanya uchaguzi wa viongozi wa taifa.