Ajali ya moto
Jeshi la zimamoto na uokoaji nchini limewataka wamiliki wa shule wanazingatia Sheria ya majengo nchini kwa kuweka idadi sawa ya wanafunzi kwenye mabweni na vyumba vya madarasa ikiwa ni pamoja na kuweka kwa usahihi vifaa vya kuzimia Moto.
Kufuatia majanga ya Moto yaliyotipotiwa hivi karibuni jijini Dar es Salaam ya kuungua Moto kwa baadhi ya Shule Eatv imezungumza na Mkaguzi Msaidizi kutoka Jeshi la zimamoto na uokoaji mkoa kizimamoto Ilala Elinimo Shang'a ambaye amewataka Wamiliki wa shule kugunga vifaa vya kung'amua Moshi ambavyo husaidia kutoa taarifa Mara baada ya kuhisi Moshi tuu kabla ya Moto.
Aidha amesisitiza wananchi kutoa Taarifa kwa wakati pindi wanapoona viashiria vya Moto huku akiwashauri wamiliki kuwa na Utaratibu wa kuajili watu ambao Wana Elimu ya kuzima Moto kuwa sehemu ya walinzi wa mifumo hiyo.
Aidha amekemea pia tabia ya watu kutotoa ushirikiano kwa wakaguzi pindi wanapopita na kwamba kila baada ya mwaka vifaa vya kuzimia Moto vinatakiwa kubadilishwa ili viweze kutoa huduma pindi yanapotokea majanga ya moto.




