Jumamosi , 10th Nov , 2018

Diwani kutoka Halmashauri ya Arumeru Jijini Arusha Nelson Mafie wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA, amekataa ombi la Mkuu wa Wilaya ya Arumeru Jerry Muro la kumtaka kuhamia Chama Cha Mapinduzi mbele ya Mkutano wa hadhara.

Mkuu wa Wilaya ya Arumeru Jerry Muro

Akizungumza kwenye mkutano wa hazara kata ya Malula alipokuwa akizungumza ya wananchi Wilayani Arumeru Jerry Muro alimtaka Diwani huyo kurejea Chama Cha Mapinduzi na kumwambia kama akihamia atafaa kuwa  Mwenyekiti wa Halmashauri hiyo.

Kama ajenda yetu ni moja kwa wananchi, tena huyu anafaa kuwa mwenyekiti wa halmashauri vipi si tutampokea huyu au mtampa masharti, jamani arudi asirudi?”  aliuliza Jerry Muro.

Akijibu Diwani huyo amesema  “nimesikia habari ya arudi au asirudi sikilizeni niwaambie nchi yetu haijengwi na watu wenye vigeugeu itajengwa na watu wenye msimamo, tunataka kuona watu wanafanya kazi kwa bidii niwaambie tu mimi siwezi kurudi CCM.”

Kumekuwa na wimbi kubwa la viongozi wa upinzani nchini kuhamia CCM, kutoka vyama vya Upinzani kwa nia ya kuunga mkono juhudi za Rais Magufuli, lakini viongozi wa upinzani wenyewe wakidai wamenunuliwa.