Jengo la maabara sekondari Geita lateketea

Jumatano , 7th Jul , 2021

Siku moja mara baada ya darasa moja lililokuwa na vifaa vya wanafunzi wa bweni katika shule ya sekondari Geita kuteketea kwa moto, usiku wa kuamkia leo Julai 7, 2021, moto mwingine tena umezuka katika shule hiyo na kuteketeza jengo la maabara. 

Sehemu ya jengo la maabara ya shule ya sekondari Geita lililoteketea kwa moto

Moto huo huo umeteketeza jengo la maabara ya Biolojia na Kemia ikiwa umepita muda wa saa 27 tu baada ya kuzuka moto kwenye darasa moja ambalo lilikuwa linahifadhia vifaa vya wanafunzi.

Mpaka sasa hakuna maafa ya vifo wala majeruhi kwenye tukio hilo, huku Jeshi la Polisi mkoani Geita likiendelea na uchungizi kufuatia matukio hayo mawili ili kubaini chanzo cha moto huo.