Alhamisi , 28th Nov , 2019

Waziri ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa TAMISEMI Selemani Jafo ameZIkemea baadhi ya Halmashauri kuendelea kuchukua mikopo kwenye benki za kibiashara kwaajili ya utekelezaji wa miradi yao.

Waziri ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa TAMISEMI Selemani Jafo

Akizungumza mara baada ya agizo la Rais Magufuli alilolitoa jana akiwa njiani kuelekea Mwanza, ambapo Jafo ametoa wiki moja kuanzia leo hadi Jumatano ijayo apate taarifa ya Halmashauri zote zilizochukua mikopo, kutoka kwenye mabenki kwadhumuni gani na kiasi gani na riba yake ikoje.

Aidha Waziri Jafo  hategemei Mkurugenzi yeyote kutoa taarifa za uongo na atakayetoa taarifa za uongo atachukuliwa hatua za kinidhamu.

Jafo amesema waliochukua na bado hawajaitumia wazirudishe kwenye mabenki walipokopa na kuanzia sasa kila kitu kisimame.