Jumatatu , 11th Apr , 2022

Barabara kadhaa zimefungwa nchini Afrika Kusini katika mahakama Pietermaritzburg wakati ambapo kesi ya rushwa inayomkabili Rais wa zamani wa nchi hiyo   Jacob Zuma ikiendelea hii leo;

Rais wa zamani wa afrika kusini Jacob Zuma

Bw. Zuma anakabiliwa na kesi za rushwa , kuingia mikataba mibovu ya kibiashara na utakatishaji fedha ikihusisha mikataba ya ununuzi silaha aliyoingia miaka ya  1990 na kampuni moja ya nchini Ufaransa.

Zuma anasema kwamba mashataka hayo yanachochoewa kisiasa.  Anatuhumiwa yeye pamoja na kampuni ya kifaransa iitwayo Thales  kupokea rushwa ya dola za kimarekani bilioni mbili, sawa na zaidi ya shilingi trilioni arobaini na sita za Kitanzania . 

Mwezi  July mwaka jana, kulitokea maandamano makubwa katika maeneo mbalimbali nchini Afrika Kusini baada ya Bw.Zuma kutiwa mbaroni.  
Amekua akikabiliwa na mashata mengi ambayo yamepelekea kuahirishwa mara kwa mara kwa kesi zake.Hii leo wanasheria wa  Zuma wameanza kumtetea mteja wao baada ya kukamilika kwa hati ya mashata kadhaa.