Mkuu wa mkoa wa iringa Bibi Amina Masenza.
Serikali mkoani Iringa imefanikiwa kuboresha sekta mbalimbali ikiwemo afya, kilimo na barabara katika kipindi cha mwaka 2010 hadi 2015.
Mkuu wa mkoa wa Iringa Bibi Amina Masenza amesema hayo leo wakati anawasilisha taarifa ya utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya Chama cha Mapinduzi (CCM) ya mwaka 2010.
Bibi Masenza amesema sekta binafsi, serikali kuu, serikali za mitaa, wananchi na wadau wameshiriki katika shughuli za maendeleo.
Aidha, mkuu wa mkoa wa Iringa amesema mkoa wa Iringa umekabiliwa na changamoto mbalimbali katika kutekeleza Ilani ya uchaguzi.
Hata hivyo, mkuu wa mkoa wa Iringa Bibi Masenza amesema serikali inatarajia kuongeza ukusanyaji wa kodi ili kutatua changamoto ambazo zinaukabili mkoa huo.