Walikamatwa Jumanne wakiwa kwenye boti mbili, baada ya boti moja kupata hitilafu za kimitambo wakati wa mazoezi, Marekani imesema.
Taarifa iliyosomwa katika runinga hiyo nchini Iran imesema wanamaji hao wameachiliwa na kuruhusiwa kuingia eneo la bahari la kimataifa baada ya kuomba radhi.
Afisa wa Marekani amethibitishia shirika la habari la Reuters kwamba mabaharia hao wameachiliwa huru.
Waliingia maeneo ya Iran bila kukusudia, taarifa kutoka kwa wanajeshi wa Revolutionary Guards iliyonukuliwa katika runinga ya taifa imesema.
Awali, kamanda wa kikosi cha wanamaji cha Revolutionary Guards, Jenerali Ali Fadavi, alikuwa amesema uchunguzi ulikuwa umeonesha hitilafu katika mitambo ya kuelekeza boti zilichangia.
"Tumethibitisha kwamba kuingia kwa wamarekani hao maeneo yetu ya bahari hakukuwa na uchokozi au kwa kusudi la kupeleleza au masuala husika,” aliambia runinga ya taifa ya Iran.

