![](http://eatv.tv/sites/default/files/styles/detailpageimg/public/news/2021/04/27/IPP TUZO.jpg?itok=Czw8HFvO×tamp=1619536654)
Kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa ITV/Radio One, Joyce Mhaville akipokea tuzo, Meneja wa Vipindi wa East Africa Radio, Lydia Igarabuza akiwa ameshikilia tuzo yake (katikati) na kushoto ni Beatrice Bandawe Mhariri Mkuu wa gazeti la Nipashe.
kupitia kalamu zao ikiwemo Wanahabari wandamizi wa Makampuni ya IPP.
Wanahabari Wanawake waliopatiwa tuzo hizo ni ishirini na tano ambao ni pamoja na Mkurugenzi wa ITV Radio One Joyce Mhavile, Meneja wa Vipindi wa East Africa Radio, Lydia Igarabuza na Beatrice Bandawe Mhariri Mkuu wa gazeti la Nipashe.
Akizungumza wakati akiwakabidhi tuzo hizo Naibu Katibu Mkuu Wizara ya habari Dkt. Ally Possi amesema kuwa katika kuelekea kilele cha maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa vyombo vya habari mwezi Mei, wanahabari wanatakiwa kufanya kazi kwa kutambua wajibu wao ni upi kabla ya kudai haki zao.
"Naomba nitoe wito kwa wamiliki wa vyombo vya habari kuhakikisha wanaendesha vyombo vyao kwa kuzingatia manufaa ya umma, kwa kutumia teknolojia za kisasa huku wakishirikisha wanawake kwani, wanawake wanaweza tena zaidi ya sana", amesema Dkt. Possi.
Kwa upande wao waliopata tuzo hizo wakatoa neno kwa Wanahabari chipukizi na masuala mazima ya uongozi ambapo wamesisitiza kufanya kazi kwa bidii na nidhamu kwa kila anayekuzunguka.