Alhamisi , 16th Oct , 2025

“Ijumaa, Oktoba 17, 2025, itakuwa siku ya mapumziko kwa heshima ya aliyekuwa Waziri Mkuu aliyeondoka, Mhe. Raila Amollo Odinga," sehemu ya tangazo huilo imesema.

Serikali ya Kenya imeitangaza siku ya Ijumaa, Oktoba 17, 2025, kuwa sikukuu ya umma kwa heshima ya aliyekuwa Waziri Mkuu Marehemu Raila Amollo Odinga.

Kupitia tangazo maalumu la gazeti la Serikali Na. 15007 lililochapishwa leo Alhamisi, Katibu wa Baraza la Mawaziri wa Mambo ya Ndani na Utawala wa Kitaifa, Kipchumba Murkomen, ametangaza tamko hilo chini ya Kifungu cha 3 cha Sheria ya Likizo ya Umma (Sura ya 110).

“Ijumaa, Oktoba 17, 2025, itakuwa siku ya mapumziko kwa heshima ya aliyekuwa Waziri Mkuu aliyeondoka, Mhe. Raila Amollo Odinga," sehemu ya tangazo huilo imesema.

Tangazo hilo linajiri huku Kenya ikijiandaa kwa mazishi ya Raila siku hiyo hiyo, kuashiria wakati mzito wa kutafakari kitaifa kwa kiongozi anayekumbukwa kwa miongo mingi ya mapambano yake ya demokrasia, mageuzi na umoja.

Tamko hilo linamaanisha ofisi za serikali, shule na biashara nyingi zitasalia kufungwa huku Wakenya wakiadhimisha siku ya kitaifa ya maombolezo na kutoa heshima zao za mwisho kwa mwanasiasa huyo mkongwe.

Bendera kote nchini Kenya zinapepea nusu mlingoti tangu Jumatano, huku vitabu vya rambirambi vikifunguliwa katika ofisi za Serikali, balozi na ofisi za chama cha ODM, chama ambacho alikuwa kiongozi wake, akiwa pia mgombea urais mara tano ambazo zote alishindwa.