
Akiwa Bandarini IGP Sirro amekutana na kufanya mazungumzo na askari wa Jeshi hilo Kikosi cha
Bandari ambapo amewataka kuhakikisha wanatimiza majukumu yao ipasavyo pamoja na kutenda haki ikiwa ni pamoja na kutoa huduma bora kwa wateja.
Hata hivyo IGP amewataka Polisi wasaidizi wanaofanya kazi bandarini hapo kushirikiana na Jeshi la Polisi ili kuendelea kudhibiti vitendo vya kihalifu vinavyofanywa na baadhi ya watu wasio waaminifu.