Jumanne , 10th Mar , 2020

Mbunge wa Hai kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Freeman Mbowe, akiwa ndani ya chumba cha Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Jijini Dar es Salaam, amesema kuwa hakuna anachokihofia na kwamba yuko tayari kwa lolote.

Mbunge wa Hai, CHADEMA, Freeman Mbowe.

Mbowe ameandika hayo leo Machi 10, 2020, kupitia ukurasa wake wa Twitter.

"Ni siku njema, msiogope! hakuna mateso yatakayozima ndoto yetu ya kutafuta demokrasia, haki na ustawi kwa wote, tusiruhusu hofu itutawale! niko tayari kwa lolote, tunaendelea kumsikiliza Hakimu! This also shall pass! Alutta continua!!" ameandika Mbowe.

Mbowe na viongozi wenzake saba pamoja na aliyewhi kuwa Katibu Mkuu wa chama hicho Dkt Vicent Mashinji, wanakabiliwa na mashtaka 13 ikiwemo ya uchaguzo.