
Jiji la Luanda mara kadhaa limekuwa likiongoza kwa gharama duniani lakini limeporomoka kufuatia kudorora kwa fedha yake.
Miji ya Zurich na Singapore imeshika nafasi ya tatu na nne katika orodha ambapo jiji la Tokyo nchini Japan limeshika nafasi ya tano.
Utafiti huo umefanyika katika miji 209 duniani, ukilinganisha gharama za upatikanaji wa huduma na ununuzi wa bidhaa ikiwemo nyumba, usafiri, chakula, nguo na burudani.
Katika utafiti huo, jiji la Kinshasa katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, DRC, limeshika nafasi ya sita ambapo jiji la Windhoek nchini Namibia limetajwa kuwa na gharama za chini kabisa duniani katika utafiti huo ukifuatiwa na Cape Town nchini Afrika Kusini.
Lakini utafiti uliofanyika mapema mwaka huu, na taasisi ya Economist Intelligence Unit, iliuorodhesha mji wa Singapore kuwa wenye gharama zaidi duninai mbele ya Zurich, Hong Kong, Geneva na Paris.