Jumamosi , 14th Jun , 2014

Serikali ya Tanzania kwa kushirikiana na serikali ya Marekani wameandaa mkutano unaolenga kujadili uhifadhi wa wanyamapori katika hifadhi zote nchini kwa kuanzia na hifadhi ya Selous.

Waziri Nyalandu akiongea na Waandishi wa Habari katika moja ya mikutano (Hawapo Pichani)

Serikali ya Tanzania kwa kushirikiana na serikali ya Marekani wameandaa mkutano unaolenga kujadili uhifadhi wa wanyamapori katika hifadhi zote nchini hususani wakianza na hifadhi ya Selous.

Hayo yameelezwa leo jijini Dar es salaam na Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe Lazaro Nyalandu wakati akipokea helikopta yenye nambari R44 Raven II 5Y- HCB ikitokea Nairobi iliyotolewa na Tajiri wa Marekani Buffet Haward nchini Kenya .

Waziri Nyalandu amesema mkutano huo utafanyika June 27 mwaka huu jijini Dar es salaam ili kuangalia namna ya kukabiliana na uhalifu wa wanyama pori