Jumamosi , 9th Mei , 2020

Waziri wa Mambo ya Nje, Prof. Palanagamba Kabudi amesema dawa ambayo Tanzania imeipokea kutoka kwa Serikali ya Madagascar, kuwa dawa hiyo haijaja kwa ajili ya matumizi badala yake ni kwa ajili ya ufaiti kwanza

Mawaziri wa Mambo ya Nje wa Tanzania (Suti nyeusi) na Madagascar wakinywa dawa inayodaiwa kuwa kinga ya Corona

Kabudi ametoa kauli hiyo wakati akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es salaam, ambapo amepokea simu za watu wengi wakiomba wapewe dawa hizo.

"Hauwezi kwenda Madagascar kuchukua dawa kwa ajili ya Watanzania wote na Ndege ya Rais, mngeniona nimeingia kwenye Ndege ya Dreamliner au Airbuss ndiyo mngejua nimechukua mzigo ili Watanzania wote wanywe." - amesema Waziri Kabudi

"Hatujaja na dawa kwa ajili ya kugawa dawa hii leo, ila ni kwa ajili ya kufanyia utafiti, nimepokea simu nyingi, SMS nyingi watu wakiniomba niwape dawa jamani mimi sina dawa, tulichokuja ni kwa ajili ya kuchunguza na kufanyiwa utafiti" ameongeza Waziri Prof. Kabudi