Jumatatu , 11th Dec , 2023

Hamas imetishia kwamba hakuna mateka hata mmoja atakayeruhusiwa kuondoka Gaza akiwa hai hadi pale matakwa yake ya kubadilishana wafungwa yatakapotimizwa.

Lakini waziri mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu amesema wanamgambo kadhaa wa Hamas wamejisalimisha na ameelezea hali hiyo kama "mwanzo wa mwisho" kwa kundi hilo.

Israel imewaamuru raia kukimbia katikati ya mji wa Khan Younis - huku afisa mmoja akisema hataki raia waliokamatwa katika "mapigano magumu" huko

Mpatanishi muhimu Qatar inasema uwezekano wa usitishaji mpya wa mapigano kati ya Israel na Hamas unapungua, lakini ameapa kuendeleza shinikizo kwa pande zote mbili.

Wakati huo huo afisa wa ngazi ya juu wa shirika la misaada la Umoja wa Mataifa ameonya kuwa nusu ya wakazi wa Gaza wana njaa, wakati mapigano yakiendelea.

Carl Skau, naibu mkurugenzi wa Shirika la Mpango wa Chakula Duniani (WFP), alisema ni sehemu ndogo tu ya vifaa vinavyohitajika ambavyo vimeweza kuingia katika ukanda huo - na watu tisa kati ya 10 hawawezi kula kila siku.

Hali katika Gaza imefanya utoaji wa huduma "karibu haiwezekani", alisema Skau.