Ijumaa , 12th Jul , 2024

Mkoa wa Geita unashika nafasi ya tatu Kwa kuwa na idadi kubwa ya watu wenye ulemavu kwa zaidi ya asilimia 10 jambo ambalo linasababisha Geita kuwa miongoni wa mikoa yenye idadi kubwa ya watu tegemezi

Hayo yamebainishwa katika maadhimisho ya siku ya idadi ya watu duniani ambapo kitaifa maadhimisho hayo yamefanyika Mkoani Geita huku ongezeko la watu Mkoani Geita likiwa ni Zaidi ya asilimia 3.

"Takwimu zinaonesha asilimia 11 ya watu wanaishi na ulemavu huku kwa mkoa wa Geita ni asilimia 10 karibu kabisa na wastani wa kitaifa takwimu hizi nikumbusha kwamba kuna haja ya mashirika kuweka mipango jumuishi ya kuwasaidia watu wenye ulemavu kwa usitawi wa taifa letuâ"- RAMADHANI HANGWA-Mchambuzi wa idadi ya watu na maendeleo kutoka NFPA

"Uwiano wa umri tegemezi ni 106.8 kati ya watu 100 wenye uwezo wa kufanya kazi juu ya uwezo wa kitaifa kati ya watu 100 watu 87.1 ni tegemezi nah ii ni takwimu za kitaifaâ" ANGELA SHAYO-Naibu katibu mkuu wa tume ya mipango

Aidha takwimu za kitaifa zinaonesha mikoa ya Mara,Mwanza na Geita ndiyo inayoongoza Kwa ukatili wa kijinsia.

"Mkoa wa Geita umeshika namba tatu katika ukatili ukifatiwa na mikoa ya mara na mwanza huku Geita ikiwa ya tatu "ANGELA SHAYO-Naibu katibu mkuu wa tume ya mipango

"Ukuaji wa ongezeko la watoto kwa mkoa wetu ni zaidi ya asilimia sita hii ni kwasababu ya jitihada za serikali kuwekeza katika huduma za afya kuna hospitali ya kanda chato imejengwa na hospitali ya rufaa ya mkoa wa Geita imejengwa na zote zinafanya kaziâ" MARTINE SHIGELA-Mkuu wa mkoa wa Geita

Naibu waziri wa wizara ya wizara ya mipango na uwekezaji Stanslaus Nyongo ambaye alikuwa mgeni rasimi katika maadhimisho hayo amesema Kasi ya ongezeko la idadi ya watu Mkoani Geita aiendani na Kasi ya ukuaji wa kiuchumi.

"Kasi ya ongezeko la watu na idadi ya watu tegemezi 106.8 kwa kila watu 100 wenye uwezo wa kufanya kazi ni wazi mkoa wetu wa Geita na mikoa mingine inakabiliwa na wimbi la ongezeko la idadi ya watu isiyoendana na kasi ya ukuaji wa uchumiâ" STANSLAUS NYONGO-Naibu waziri wizara ya Mipango na uwekezaji