Jumatano , 18th Dec , 2019

John Henderson (106) na mkewe Charlotte Curtis (105), ni binadamu ambao wanashikilia rekodi ya kuwa kwenye mahusiano kwa muda mrefu zaidi duniani na wanategemea kufanya kumbukumbu ya kutimiza miaka 80 ya ndoa yao, ifikapo siku ya Disemba 22, 2019.

Wanandoa John Henderson (106) na mkewe Charlotte Curtis (105).

Wawili hao walifunga ndoa mwaka 1939, baada ya kuwa katika mahusiano kwa muda wa miaka 4, ambapo walikutana katika chuo cha Texas Austin, mwaka 1934, wakati wanasomea mambo ya elimu kuhusiana na wanyama.

Akizungumzia sababu ya kukutana kwao na kuwa wapenzi John Henderson amesema "Mke wangu Charlotte alikuwa anaangalia sana bega langu na kutabasamu akiniona, ndipo nilipojua alitaka tutoke mtoko tukiwa pamoja na tukaanzisha mahusiano".

Licha ya wapenzi hao kuishi kwa muda mrefu, hawabahatika kupatahata mtoto kwenye maisha yao na wamesema hawaoni tatizo lolote, kwani hata siku ya ndoa yao walihudhuria watu wawili tu.

Aidha wameeleza sababu iliyofanya waishi muda mrefu zaidi ni pamoja na kuzingatia kiasi cha chakula wanachokula na kutokunywa sana vinywaji,pamoja na kufanya mazoezi ya mara kwa mara.