
Mzee Meshuku Mapi, wakati wa uhai wake
Mzee Meshuku maarufu kwa jina la Mzee Laibon alifariki Dunia Aprili 10 na alizikwa Aprili 15, 2020, katika Kijiji cha Esilalei ,huku wito ukitolewa kwa wanafamilia na jamii ya wafugaji, kumuenzi kwa kudumisha na kuendeleza yale yote aliyo kuwa ameyaanzisha.
Mzee Laibon katika hali isiyo ya kawaida kwa wazee wa umri na aina yake, alijiunga na Kanisa la KKKT na kubatizwa hii ikimanisha alifanikiwa kuwa muumini halali wa Kanisa hilo.
Mzee Laibon alizaliwa Aprili 24, 1914, na ameacha wake sita, ambapo inadaiwa kuwa mke wa kwanza alimuoa akiwa na miaka 30.
Aidha wakati wa uhai wake, alianzisha shule katika viwanja vya Boma lake iliyowasaidia watoto walio karibu na eneo hilo kupata elimu, licha ya kuwa karibu asilimia 90 ya wanafunzi wote ni watoto na wajukuu wake.
Tazama video hapa chini ili kushuhudia mazishi yake.