Mkurugenzi wa Usimamizi wa Uchumi wa Mamlaka ya Udhibiti wa Nishati na Maji (Ewura)Felix Ngamlagosi (kulia) akitangaza bei mpya za mafuta
Kutoka na Kushuka kwa thamani ya shilingi ya Tanzania ei ya Petroli imeendelea kupanda baada ya mamlaka ya udhibiti wa huduma za Nishati na Maji EWURA, kutangaza ongezeko la sh. 11 wakati Dizeli ikipanda kwa shilingi 23.
Kwa mujibu wa viwango vilivyotangazwa jana na EWURA, bei ya petroli imepanda kutoka sh. 1755 hadi shilingi 1866 wakati dizel ikipanda kutoka shilingi 1672 hadi kufikia 1695 na hii ikiwa ni mara ya pili katika miezi miwili EWURA kupandisha bei ya bidhaa hiyo.
Katika taarifa yake kwa vyombo vya habari bei hiyo elekezi itaanza kutumika kwa mkoa wa Dar es Salaam na mikoa mingine na zitaanza rasmi kutumika kuanzia leo Jumatano
Aidha taarifa hiyo imefafanua kuwa sababu ya kupanda kwa bei hizo ni kutokana na mabadiliko ya bei ya mafuta katika soko la dunia na kushuka kwa thamani ya shilingi dhidi ya dola ya marekani.
EWURA imesema kuwa kumekuwa na kushuka bei hata katika soko la ndani lakini za hapa zitaakisi kushuka huko katika kipindi cha miezi miwili.