Jumatano , 6th Jan , 2016

Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji(EWURA),imepunguza bei ya mafuta ambayo itaanza kutumika rasmi kuanzia leo.

Mkururugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA),Felix Ngamlagosi akisisitiza jambo wakati wa mkutano na waandishi wa habar

Akiongea na Waandishi wa habari Jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka hiyo Felix Ngamlagosi, amesema kuwa Januari mwaka huu bei za rejareja za mafuta ya petroli zimepungua kwa shilingi 79 sawa na asilimia 4.01, mafuta ya dizeli sh. 76 sawa na asilimia 4.20 mafuta ya taa kwa sh. 66 sawa na asilimia 3.73

Ngamlagosi ameongeza kuwa Kupungua kwa bei ya mafuta kumetokana na kushuka kwa bei ya mafuta kwenye soko la dunia, kushuka gharama za usafirishaji na uletaji wa bidhaa za mafuta kutoka nje.

Aidha mkurugenzi huyo amesema kuwa kampuni za mafuta zipo huru kuuza bidhaa hizo kwa bei ya ushindani ili mradi bei hizo ziwe chini ya bei kikomo iliyowekwa na serikali.