Jumanne , 8th Sep , 2015

Watanzania wametakiwa kumuepuka na kumuogopa kama ukoma mtu yeyote bila kujali wadhifa wake anayewania madaraka hasa wa kuliongoza taifa kwa kutumia udini kwa kuwa ataligawa taifa.

Katibu Mkuu mstaafu wa chama cha Mapinduzi CCM, Mh. Yusuph Makamba

Wakizungumza Mkoani Tanga Katibu Mkuu mstaafu wa chama cha Mapinduzi CCM, Mh. Yusuph Makamba na Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi ccm Alhaji Bulembo na kusema tume ya taifa na waangalizi wa Kimataifa waanze kuzifuatilia kauli hizo zilizoanza kutolewa na baadhi ya viongozi wanaowania nafasi hizo.

Viongozi hao waandamizi wamesema kuwa mtu yoyote anayetumia udini hafai kuliongoza taifa kwa kuwa udini ni mbegu mbaya ya uchochezi inayoweza kuleta machafuko na kusababisha amani iliyojengwa kwa muda mrefu kutoweka.

Wakati huo huo jana Kampeni za Mgombea huyo ziliekekea mkoani Tanga ambapo watanzania wametakiwa kumuepuka na kumuogopa kama ukoma mtu yoyote bila kujali wadhifa wake anayewania madaraka hasa wa kuliongoza taifa kwa kutumia udini kwa kuwa ataligawa taifa.

Wakizungumza Mkoani Tanga Katibu Mkuu mstaafu wa chama cha Mapinduzi CCM, Mh. Yusuph Makamba na Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi CCM Alhaji Bulembo na kusema tume ya taifa na waangalizi wa Kimataifa waanze kuzifatilia kauli hizo zilizoanza kutolewa na baadhi ya viongozi wanaowania nafasi hizo.