Sezbera amesema pamoja na tatizo la uhaba wa fedha linaoikabili jumuiya hiyo imefanikiwa kwa kiasi kikubwa kukabiliana na changamoto za kisiasa kiuchumi na kijamii na malengo yaliyowekwa yanaendelea kufikiwa likiwemo la kupunguza kutegemea misaada toka kwa wahisani.
Akizungumzia hatua iliyofikiwa katika utekelezaji wa malengo ya jumuiya hiyio katika kipindi cha mwaka 2014/2015 Dkt Sezbera amesema utegemezi wa wahisani unaendelea kupungua na uchumi na ushirikiano unaimarika kwa nchi wanachama na kwa wananchi kwa ujumla .
Kuhusu changamoto za kisiasa ikiwemo ya vuguvugu la uchaguzi linalozikabili nchi za Burundi na Tanzania Dkt. Sezbera amesema ni za kawaida na pia jumuiya inaendelea kushirikiana na nchi husika kuhakikisha inafanya kila linalowezekana kuhakikisha kuwa changamoto zote zinazojitokeza zinatatuliwa kwa njia ya mazungumzo .
Akizungumzia hatua iliyofikiwa katika kuimarisha uchumi dr, sezbera amesema pamoja na kuwepo kwa changamoto katika sekta za mbalimbali za uchumi ikiwemo ya utalii amesema jitihada zinaendelea na baadhi zimeshapata ufumbuzi na zingine zinaendelea kutafutiwa majawabu .
Akizungumzia suala la usalama Dkt Sezbera amesema hali ni shwari na jitihada za kuhakikisha kuimarisha utulivu na amani katika nchi wanachama na majirani zake ikiwemo nchi Sudani Kusini zinaendelea sambamba na mazungumzo ya kuiwezesha nchi hiyo kujiunga a na jumuiya.