Alhamisi , 28th Feb , 2019

Kamanda wa Polisi Kinondoni, Mussa Taibu amesema Msanii, Dudu baya anashikiliwa kituo cha polisi Oysterbay kwa mahojiano zaidi kutokana na kuchapisha video zenye lengo la kumdhihaki marehemu Ruge Mutahaba.

Picha ya msanii Dudu Baya.

Akizungumza na www.eatv.tv, Kamanda Taibu amesema kuwa mtuhumiwa huyo alikamatwa jana na anashikiliwa katika kituo cha Polisi cha Osterbay, na wanaendelea na uchunguzi.

"Huyu mtu tayari tunaye na tunafanya uchunguzi kuhusiana na kile kilichotokea kutokana na kuonyesha dhihaka dhidi ya marehemu Ruge Mutahaba, tukikamilisha uchunguzi wetu tutakuja na majibu kwa umma", amesema Kamanda Taibu.

Jana Waziri wa Habari sanaa utamaduni na michezo Dkt. Harrison Mwakyembe aliagiza Jeshi la Polisi nchini pamoja na Baraza la Sanaa la Taifa kushughulika na msanii huyo kutokana na maneno aliyoyatoa mtandaoni kuhusu marehemu ambaye alikuwa ni Mkurugenzi wa Vipindi na Uzalishaji wa Clouds.

Bofya link hapo chini kumsikiliza Kamanda Taibu akifunguka zaidi.