Jumatatu , 4th Jul , 2016

Rais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, Dkt. Ali Mohammed Shein, amesema serikali yake itaendelea kuchukua hatua za makususdi katika kuhakikisha sekta ya elimu inaimarika.

Rais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, Dkt. Ali Mohammed Shein,

Akizungumza mwishoni mwa wiki visiwani humo wakati akipokea msaada wa madawati 50 kutoka kwa Masheikh wa Jumuiya ya Khoja Shia Ithna Sharia amesema kuwa SMZ inathamini sekta ya elimu ndio maana ilianza kutoa elimu tangu wakati wa Hayati Abeid Amani Karume.

Rais Shein amesema katika kuimaarisha sekta hiyo wananchi na taasisi mbalimbali wanapaswa kujitokeza kuiunga mkono sera ya elimu bure ili izidi kuimarika.

Dkt. Shein amesema kuwa katika Ukanda wa Afrika Mashariki na Kati Zanzibar, ina historia kubwa ya elimu ya dini na dunia kwani ndio nchi ya mwanzo kutoa elimu kuanzia miaka ya 1890 kwa elimu ya dini na 1905 walianza kutoka elimu ya dunia.