Makamu wa Rais Dkt. Philip Mpango akizungumza na waombolezaji wakati wa kuaga mwili wa Mkuu wa Majeshi Mstaafu, Jenerali David Bugozi Musuguri katika Hospitali Kuu ya Jeshi Lugalo Jijini Dar es salaam tarehe 01 Novemba 2024.
Makamu wa Rais amesema hayo wakati wa kuaga mwili wa Mkuu wa Majeshi Mstaafu, Jenerali David Bugozi Musuguri katika Hospitali Kuu ya Jeshi Lugalo Jijini Dar es Salaam.
Ametoa rai hasa kwa vijana wa Tanzania kuipenda nchi na Jeshi la Tanzania kwa moyo wote na kuwa tayari kuilinda Tanzania kwa gharama yoyote kama alivyofanya Jenerali (Mstaafu) Musuguri.
Makamu wa Rais amesema makamanda na wapiganaji waliopewa dhamana ya uongozi katika Jeshi hawana budi kuendelea kufuata mfano bora uliyoachwa na Jenerali Mstaafu David Musuguri.
"Hayati Jenerali (Mstaafu) Musuguri alilipenda sana Jeshi maisha yake yote, alitamani vijana wengi wajiunge na Jeshi na alifanikiwa sana kuwaandikisha jeshini vijana wengi amesema alikuwa mwalimu na mlezi makini wa askari vijana aidha, alipopewa jukumu la kuongoza Jeshi la Wananchi wa Tanzania alifanya jitihada kubwa kulijenga na kuliendeleza Jeshi na kulifanya kuwa kati ya majeshi bora na imara barani Afrika ndiyo maana Jeshi la Idd Amin lilipovamia kipande cha ardhi ya Tanzania lilidhibitiwa kutoka kwa Jeshi la Tanzania likiongozwa na Jenerali Mstaafu Musuguri," amesema Makamu wa Rais
Makamu wa Rais ametoa salamu za pole kwa niaba ya Rais Samia Suluhu Hassan, na serikali nzima kwa Mkuu wa Majeshi na Jeshi la Wananchi wa Tanzania kwa ujumla, familia, ndugu wa marehemu na Watanzania wote kwa msiba huo mkubwa kwa Taifa. Amesema serikali inaiombea faraja familia ya Musuguri na wote walioguswa na msiba huo.