Alhamisi , 3rd Mar , 2016

Mkutano wa 17 wa viongozi wa nchi Wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki umemalizika Mjini Arusha ambapo pamoja na mambo mengine umemuongezea Muda wa Mwaka mmoja rais John Pombe Magufuli kuwa mwenyekiti wa Jumuiya hiyo.

Viongozi wakuu wa Nchi za Afrika ya Mashariki wakisimama wakati wimbo wa umoja wa nchi hizo ukipigwa katika mkutano wa 17 wa EAC

Akiongea katika Mkutano huo Mwenyekiti huyo alieongezewa Muda Raisi Magufuli amesisitiza maamuzi kadhaa ya msingi ikiwemo suala la kuimirsha suala la viwanda ili kuweza kukuza ajira na kuongeza thamani ya Mazao na kukuza pato la taifa la nchi husika.

Aidha Mkutano huo umezingumzia uimarishaji biashara katika jumuiya hiyo pia na kumekuwa na tukio kubwa la kuzinduliwa kwa passport mpya ambayo imetengenezwa katika mfumo wa kieletroniki.

Mkutano huo pia umethibitisha Sudani Kusini kuwa Mwanachama mpya wa Jumuiya ya Afrika Mashariki na kuzifanya nchi wanachama kuwa sita ambazo ni Tanzania,Kenya,Uganda, Rwanda, Burundi na Sudani Kusini.

Halikadhilika katika Mkutano huo umefanyika uchaguzi wa viongozi kadhaa ambao wanachukua majukumu mbalimbali ikiwemo katibu mkuu mpya wa jumuiya hiyo pamoja na msajili wa mahakama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki.