Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete Akilihutubia Bunge.
Katika hotuba yake hiyo Rais Kikwete aliezea mafaniko yaliyopatikana katika sekta mbalimbali ikiwemo ya Nishati ya Umeme,Gesi, Viwanda, Elimu, Afya, Taasisi za Fedha na Teknolojia za Mawasiliano.
Aidha Rais Kikwete amesema katika kipindi chake kwa nia ya Kusogeza huduma kwa jamii Serikali ilianzisha mikoa mipya minne, Wilaya 19 na halmashauri 45 pamoja na kata na vijiji na mwaka huu wameanzisha mkoa mpya mmoja wa Songwe pamoja na wilaya mpya sita.
Ameongeza kuwa katika kwa nia ya kuongeza uwajibikaji ufanisi na kupunguza malalamiko Mahakamani serikali imetenganisha kazi ya upelelezi na kazi ya kuendesha mashtaka ili kutoa nafasi ya kesi nyingi kusikilizwa.
Tanzania imekuwa kati ya nchi 10 Afrika zinazokua kiuchumi ambapo katika kipindi cha miaka kumi pato la taifa limekuwa kwa asilimia 7 kutokana na sera za uchumi zinazogusa wananchi wa kawaida.
Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete amesema kuwa kati ya nchi kumi Tanzania ni ya 7 na pia ipo katika mataifa 20 dunia ambayo uchumi wake unakua kwa kasi.
Rais Kikwete ameongeza kuwa Pato ghafi la Taifa limeongeza mara tatu toka trilion 14 .1 mwaka 2005 hadi trilion 79 huku pato la wastani la mwananchi wa kawaida nalo limeongezeka toka laki nne 44 elfu na 30 hadi milioni 1 laki saba na 24 elfu.
Katika hatua nyingine wakati akizindua Jengo la CCM mweyekiti huyo wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) amekitaka chama hicho kuzitumia rasilimali zake zilizopo ili waweze kupata mtaji wa kukiendesha chama hicho bila kutegemea wahisani.
Amesema kitendo cha CCM kujenga ukumbi huo ni ishara kwamba wanaweza kuzitumia rasilimali zao vizuri kwa ajili ya kukiondoa chama hicho na utegemezi wa fedha za wahisani ambazo mara nyingine huwa zinawagharimu.
Amesema kwa mkoa wa Dar es Salaam peke yake chama hicho kina viwanja 420 ambavyo havijaendelezwa lakini vinatumika kama maegesho ya magari ambapo mapato yote yanayopatikana yanakwenda kwa walinzi wa magari hayo.
Insert.. Jk rasilimali za ccm zitumike
Kwa upande wake balozi wa China nchini, Lu Youqing amekipongeza chama cha mapinduzi kwa hatua waliyoifikia na kusema kuwa nchi hizo mbili zimekuwa katika urafiki wa kudumu na kwamba urafiki huo utaendelea kuwepo siku zote.