
Baadhi ya nyumba zinazotajwa kuchomwa moto
Kwa mujibu wa Mkuu huyo wa Wilaya, ofisi yake ilishatoa maelekezo kwa wakazi wa eneo hilo kuhama eneo la hifadhi ya misitu kwa kile walichokidai walisababisha uharibifu wa misitu na vyanzo vya maji kwenye eneo hilo la hifadhi.
Akizungumza na www.eatv.tv Mzee amekiri kupokea madai ya nyumba hizo kuchomwa moto na badala yake ameagiza timu maalum kufatilia taarifa hiyo.
“Kusema kwamba nilikuwepo sio sahihi, japo nimetuma timu kwa ajili ya kwenda kuchunguza madai ya wananchi kuondolewa kwa nguvu kwa sababu mwaka jana mwezi septemba 2017 tulifika pale tukawaambia waondoke na walielewa na walikubali”, amesema Seleman Mzee.
“Serikali ya kijiji na halmashauri walishirikiana kuhakikisha wanaondoka, lakini ilipokuja taarifa kwamba watu wamebomolewa kwa nguvu, ilikuwa lazima waondoke hata kama wangebomoa wenyewe”, ameongeza Mkuu huyo wa Wilaya.