Ijumaa , 2nd Oct , 2015

Mamlaka ya maji safi na maji taka jijini Dar es salaam DAWASCO imezindua kampeni ya Mama Tua Ndoo ya maji kichwani kampeni ambayo inalenga kurahisisha upatikanaji wa maji safi na salama katika jiji la Dar es salaam.

Mkurugenzi wa DAWASCO Mhandisi Cyprian Luhemeja

Akiongea katika uzinduzi huo mkurugenzi wa DAWASCO Mhandisi Cyprian Luhemeja amesema kuwa kampeni hiyo inawakusanya wauza maji wote wa jiji la Dar es salaam na kuwapa usajili wa kisheria ili iwe rahisi kuwawezesha kusambaza maji kwa ukaribu zaidi.

Luhemeja ameongeza kuwa kuanzia hii leo mpaka Novemba 30 itakuwa ni kipindi cha usajili na wafanyabiashara ya maji ili waweze kunufaika na biashara hiyo pamoja na kuwa kisheria na sio kwa kujifichaficha kama ilivyokuwa awali.

Ameongeza kuwa kila kaya itengewe visima vya maji kwa lengo la magari yaliyosajiliwa kuchukua maji kwenye visima hivyo mpaka majumbani kama sehemu ya kurahisisha huduma ya maji.