Jumapili , 23rd Aug , 2020

Wakazi wa Mtaa wa Bwawani Makumbusho Jijini Dar es Salaam wameulalamikia uongozi wa Mamlaka ya Maji Safi na Maji Taka (Dawasa) kwa kushindwa kutatua changamoto ya kupasuka kwa mabomba ya maji mtaani hapo na kupelekea adha ya maji kujaa mtaani hadi mengine kuingia ndani.

Maji taka yakiwa yanaendelea kutoka katika mtaa wa Bwawani

Wakizungumza na Kurasa wakazi hao wamesema kuwa mara kadhaa wameuandikia barua uongozi huo kushughulikia kero yao hiyo lakini umekuwa mzito katika kutatua kero hiyo ya kupasuka kwa mabomba ya maji.

Wakazi hao wamesema kuwa maji hayo yamekuwa hatari kwa watoto wadogo ambao huchezea maji yaliyotuama hivyo kuwa hatarini kupata maradhi, pia yanageuka kuwa mazalia ya mbu.

“Mara kadhaa tunaandika barua kwa uongozi ila wanakuja kufanya marekebisho madogo tu na hali inarudi kama kawaida, tunaomba watuchimbie mitaro ili maji yawe yanaingia huko sio kama ambavyo yanaingia ndani tunapata tabu sana” amesema Bi. Merida.