Jumamosi , 16th Apr , 2022

Daktari mmoja nchini Scotland, Krishna Singh (72) amekutwa na hatia ya makosa 54 ya unyanyasaji wa kingono dhidi ya Wanawake. 

Miongoni mwa makosa hayo ni kuwabusu, kuwapapasa wagonjwa 48 wakati alipokutana nao katika mazingira mbalimbali ya matibabu.

Daktari huyo anadaiwa kuyafanya makosa hayo kwa zaidi ya miaka 35 iliyopita ikiwa ni kati ya Februari 1983 na Mei 2018.

Jaji anayesimamia kesi hiyo Lord Armstrong amesema hukumu itatolewa mwezi ujao.